Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
TANGAZO LA DHARURA - KUZIMWA KWA MTAMBO WA UZALISHAJI MAJI RUVU JUU
10 Jan, 2025 Pakua
TANGAZO LA DHARURA - KUZIMWA KWA MTAMBO WA UZALISHAJI MAJI RUVU JUU

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inawatangazia wateja na Wananchi wanaohudumiwa na mtambo wa kuzalisha maji Ruvu juu kuwa, kutakuwa na ukosefu wa huduma ya maji kwa muda wa saa 8  kwa Siku ya Ijumaa, Januari 10, 2025

Muda; kuanzia Saa 3 Asubuhi hadi Saa 11 jioni.

Sababu: Kuruhusu maboresho ya miundombinu  umeme katika maeneo ya Ruvu darajani.
 
Maeneo yatakayoathirika ni; 
Chalinze, Mboga,Ruvu Darajani, Ruvu JKT, Vigwaza, Mlandizi, Mbwawa, Visiga, Maili 35, Misugusugu, Kongowe, Soga, Miembe Saba, Kwa Mfipa, Mwendapole, Tanita, Kwa Mathias, Kwa Mbonde, Picha ya Ndege, Lulanzi, Kibaha, Kiluvya, Kibamba, Mbezi, Magari Saba, Mbezi Inn, Mbezi, Kimara, Tabata, Segere, Kinyerezi, Kisukuru, Bonyokwa, Msigani, Maramba Mawili, Kimara B, Kimara Korogwe, Bucha, Baruti, Ubungo, Magomeni, Ukonga, Uwanja wa Ndege, Kiwalani, Vingunguti, Gongo la Mboto, Pugu na Kisarawe

Tunaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza.

Wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja 0800110064 (bure) au 0735 202-121 (WhatsApp Tu)

Imetolewa na 
Kitengo cha Mawasiliano