TANGAZO LA DHARURA - KUZIMWA KWA MTAMBO WA UZALISHAJI MAJI RUVU JUU KWA SAA 24
![TANGAZO LA DHARURA - KUZIMWA KWA MTAMBO WA UZALISHAJI MAJI RUVU JUU KWA SAA 24](https://www.dawasa.go.tz/uploads/announcements/72c5e583950f71485d36fa20580c6d50.jpeg)
TANGAZO LA DHARURA
KUZIMWA KWA MTAMBO WA UZALISHAJI MAJI RUVU JUU KWA SAA 24
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inawatangazia Wateja na Wananchi wanaohudumiwa na mtambo wa kuzalisha maji Ruvu juu kuwa, kutakuwa na ukosefu wa huduma ya maji kwa muda wa saa 24 kuanzia siku ya Jumanne Desemba 10, 2024 kuanzia Saa 12 jioni hadi Saa 2 Asubuh ya Desemba 11, 2024
Sababu: Kuruhusu matengenezo ya bomba kubwa la inchi 40 linalopokea na kupeleka maji kwa Wananchi.
Maeneo yatakayoathirika ni;
Chalinze, kijini cha Mboga, Ruvu Darajani, Ruvu JKT, Vigwaza, Mlandizi, Mbwawa, Visiga, Maili 35, Misugusugu, Kongowe, Soga, Miembe Saba, Kwa Mfipa, Mwendapole, Tanita, Kwa Mathias, Kwa Mbonde, Picha ya Ndege, Lulanzi, Kibaha, Kiluvya, Kibamba, Mbezi, Magari Saba, Mbezi Inn, Mbezi, Kimara,Tabata, Segere, Kinyerezi, Kisukuru, Bonyokwa, Msigani, Maramba Mawili, Kimara B, Kimara Korogwe, Bucha, Baruti, Ubungo, Magomeni, Ukonga, Uwanja wa Ndege, Kiwalani, Vingunguti, Gongo la Mboto, Pugu na Kisarawe
Wananchi wanashauriwa kuhifadhi maji kwa wingi na kuyatumia kwa matumizi muhimu zaidi.
Wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja 0800110064 (bure) na 0735 202-121 (WhatsApp Tu)
Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano