TANZIA
							
							
							
							
							
						
					
                            
                                 26 Feb, 2025
                            
                                                        
                                 Pakua
                            
                                                    
                    
                    TANZIA
BARIKI LAMSON NZOWA
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) anasikitika kutangaza kifo cha Ndg. Bariki Lamson Nzowa (DAWASA Mtoni) aliyekuwa Dereva Mwandamizi, kilichotokea tarehe 24/02/2025 saa 01:00 usiku kwa ajali ya pikipiki eneo la Tabata - Maji Chumvi, Dar es Salaam.
Kwa sasa msiba upo nyumbani kwa Marehemu Tabata - Kisukuru kwa Mkuwa, Dar es Salaam.
DAWASA tunaungana na familia ya marehemu katika kuomboleza msiba huu mzito.
Bwana Ametoa na Bwana Ametwaa, Jina la Bwana Lihimidiwe
            