TANZIA
04 Mar, 2025
Pakua

TANZIA
DEVOTHA ASANTE MPAKA
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) anasikitika kutangaza kifo cha Ndg. Devotha Asante Mpaka (DAWASA Ilala) aliyekuwa Msaidizi wa Ofisi, kilichotokea tarehe 3/3/2025 saa 02:30 Asubuhi katika Hospitali ya Regency eneo la Upanga, Dar es Salaam.
Mazishi yatafanyika nyumbani kwa wazazi wa Marehemu, Muleba mkoani Kagera.
DAWASA tunaungana na familia ya marehemu katika kuomboleza msiba huu mzito.
Bwana Ametoa na Bwana Ametwaa, Jina la Bwana Lihimidiwe