Wizara ya Maji

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)

TIRA Logo
UTEKELEZAJI WA MRADI WA UJENZI WA BWAWA LA MAJI KIDUNDA
25 Nov, 2025 Pakua
UTEKELEZAJI WA MRADI WA UJENZI WA BWAWA LA MAJI KIDUNDA

UTEKELEZAJI WA MRADI WA UJENZI WA BWAWA LA MAJI KIDUNDA

● Utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Bwawa la Maji Kidunda una lengo la kuhifadhi maji kwajili ya matumizi kipindi cha kiangazi na kuhakikisha utiririshaji wa maji katika mto Ruvu kwa kipindi chote cha mwaka.

● Mpaka sasa mradi umefikia asilimia 33.6 za utekelezaji wake na kukamilika kwake utanufaisha wakazi takribani 7,408,675 wa Mikoa ya Dar Es Salaam na Pwani.

● Mradi unahusisha Ujenzi wa bwawa lenye uwezo wa kuhifadhi maji Lita bilioni 190, Mtambo wa kuzalisha umeme megawati 20 kwa siku, ujenzi wa barabara kwa kiwango cha changarawe kilomita 75 kutoka Ngerengere hadi Kijiji cha Kidunda, ujenzi wa njia ya umeme kilomita 101 toka Kidunda hadi Chalinze.