BAGAMOYO WAONGEZEWA WIGO WA HUDUMA
Elimu ya Udhibiti Upotevu wa Maji yapewa msukumo zaidi
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)imeendelea na utekelezaji wa mkakati wa Serikali wa kuhakikisha wananchi wote wa Dar es Salaam na Pwani wanafikiwa na huduma ya maji kwa kugawa vifaa vya maunganisho ya maji kwa wananchi kwa lengo la kusogeza huduma karibu na wateja.
Vifaa hivyo vimetolewa kwa wananchi 61 wa Kata 7 za Bagamoyo ambazo ni Dunda, Kiromo, Zinga, Yombo, Magomeni, Kisutu na Nianjema. Pamoja na mitaa yake ikiwemo, nianjema A, B,C, shimo la punda, kidongo chekundu, mti wa boni, kimara ng'ombe, Sanzale, epifani, mtaa wa stand, block p, kisutu, kaole, kiromo, Kitopeni, migude, ukuni, hospitali ya wilaya, kwa zakaria na igo.
Utoaji wa vifaa vya maunganisho mapya ya maji umeenda sambamba na utoaji wa elimu ya matumizi bora ya maji, pamoja na kushirikisha kuzuia upotevu wa maji katika makazi yao kwa kulinda usalama wa miundombinu ya maji.
Mamlaka inawataka wananchi kutumia njia sahihi za kuwasiliana na Mamlaka ikiwemo namba ya huduma kwa wateja 181(Bure)na (0735 202121) Whatsapp tu.
