Wizara ya Maji

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)

TIRA Logo
MAGOMENI, MANZESE NA SINZA WANUFAIKA NA HUDUMA YA MAJI
16 Sep, 2026
MAGOMENI, MANZESE NA SINZA WANUFAIKA NA HUDUMA YA MAJI

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kupitia mkoa wa kihuduma Magomeni imeendelea na zoezi la utoaji vifaa vya maunganisho mapya ya huduma ya majisafi kwa wananchi wa maeneo ya Magomeni, Manzese, Kigogo, Mburahati, Mzimuni na Sinza ikiwa ni jitihada za Serikali za kuboresha upatikanaji wa maji safi na salama.

Zoezi hilo limetekelezwa na DAWASA Mkoa wa kihuduma Magomeni, ambapo zaidi ya wateja wapya 49 kutoka mitaa ya mitaa ya Mwinyimkuu, Manzese uzuri, Tandale kwa mtogole, Sinza kwa remmy wamekabidhiwa vifaa vya maunganisho ya majisafi ili kuwawezesha kupata huduma hiyo katika makazi yao.

Mbali na kugawa vifaa hivyo, DAWASA pia imetoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kutunza miundombinu ya maji, kulipa bili kwa wakati na kushiriki katika juhudi za kudhibiti upotevu wa maji ili kuhakikisha huduma inaendelea kuwa endelevu.

Wananchi wamehimizwa kuendelea kushirikiana na mamlaka hiyo kwa kutoa taarifa kuhusu changamoto za huduma na kupata ufafanuzi kupitia namba 0735 451 862 (DAWASA Magomeni) au 181 namba ya huduma kwa wateja, bila malipo.