BAKARI MAKILAGI MFANYAKAZI BORA 2025

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imefanya uchaguzi wa mfanyakazi bora kwa mwaka 2025 na kumchagua Mtumishi Bakari Makilagi kuiwakilisha Mamlaka katika Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi (Mei Mosi) inayoadhimishwa tarehe 1 Mei kila mwaka.
Akizungumza wakati wa zoezi la upigaji kura kwa niaba ya Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu ,Mhandisi Ramadhani Mtindasi amesisitiza watendaji kuchagua mfanyakazi kazi bora katika majina kumi yaliyowasilishwa ya watumishi kutoka maeneo mbalimbali ya kihuduma ya DAWASA.
Baada ya uchaguzi huo, Afisa rasilimali watu wa Mkoa wa kihuduma DAWASA Kinyerezi Ndugu Bakari Makilagi aliibuka kuwa mfanyakazi bora wa Mamlaka kwa mwaka 2025 kwa kupata kura 472 kati ya kura 1322 zilizopigwa.
Maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani kitaifa yanategemea kufanyika Mkoa wa Singida yakibeba kauli mbiu ya "Uchaguzi mkuu 2025 utuletee viongozi wanaodai haki na maslahi ya wafanyakazi, Sote tushiriki"