Wizara ya Maji

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)

TIRA Logo
DAWASA YAWAFIKIA WANANCHI KUELEKE SIKU YA WANAWAKE DUNIANI
05 Mar, 2026
DAWASA YAWAFIKIA WANANCHI KUELEKE SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imefungua dawati la huduma kwa wateja katika mtaa wa Bwawani, Stand ya Makumbusho kwa lengo la kuwafikia wananchi kutatua changamoto na kupokea maoni juu ya uboreshaji huduma ya maji.

Akizungumzia katika Dawati hilo Afisa Huduma kwa Wateja DAWASA, Ndugu Veronica Sebastian amesema Mamlaka imefungua dawati hili katika kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Ili kuwafikia wananchi mtaani kutatua changamoto za maji hususani wakinamama ambao kwa asilimia kubwa ndio watumiaji wa maji.

"Katika dawati letu hapa stendi ya mabasi Makumbusho, mtaje atapata huduma zote zinazotolewa na Mamlaka, ikiwemo maunganisho ya maji, changamoto za bili, uvujaji lakini atapata elimu ya njia za malipo huduma za DAWASA, zaidi tunapokea maoni juu ya uboreshaji wa huduma ya maji kutoka kwa wananchi wenyewe," amesema Ndugu Veronica.

Veronica amesema dawati hili litakuwa katika stendi ya Makumbusho kwa siku 5 kwanzia leo rarehe 3.3. 2026 hadi 7.3. 2026 na kuwasihi wananchi hususani kina mama kujitokeza kwa wingi kupatiwa huduma.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Mtaa wa Bwawani, Ndugu Mahmood Tonsa amesema hatua hii ya DAWASA kuwafata wananchi mtaani na kuwasikiliza ni mfano wa kuigwa huku akiwasisitiza wananchi hususani wanawake kufika katika dawati hilo kutatuliwa changamoto zao.

"Tunashukuru kwa huduma ya maji tunayoendelea kuipata hususani mtaa wetu huu wa Bwawani, zipo changamoto ndogondogo ambazo wananchi wamekuwa wakilalamikia, hii ni nafasi yao kufika katika banda hili kutatuliwa changamoto, binafsi nimefika hapa elimu na huduma inayotolewa kuhusu huduma ya maji ni nzuri sana," amesema Tonsa.

Ndugu Kidani Magwille, Mkazi wa Sinza A amesema ameridhishwa na huduma zinazotolewa katika dawati hilo na kuwaasa wananchi wajitokeze kwa wingi kupatiwa huduma

"Binafsi nilikuja na changamoto ya bili ya maji na mita yangu kuwa na ukungu, nafurahi kwakua changamoto yangu imetatuliwa hapa hapa, huu ni msaada mkubwa kwetu wananchi hasa sisi watumiaji wakubwa wa maji ambao ni wanawake," amesema Ndugu Kidani.