BIASHARA SAA 24 KARIAKOO, DAWASA MGUU SAWA

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imeanza utekelezaji wa agizo la utoaji huduma Saa 24 katika eneo la Kariakoo jijini Dar es salaam.
Utoaji huduma saa 24 umelenga kutoa nafasi kwa wafanyabiashara na wageni kutoka nje ya nchi kuweza kufanya biashara bila kikwazo chochote.
Katika kilele cha uzinduzi wa biashara saa 24 uliofanywa na Mkuu wa Mkoa huo, Albert Chalamila Februari 27, 2025 alisema wamejipanga vyema kuhakikisha hilo linafanikiwa bila kikwazo.
Kutokana na hilo, Mkurugenzi wa huduma za Usafi wa Mazingira DAWASA, Mhandisi Lydia Ndibalema amesema Mamlaka inachagiza adhma ya Serikali ya awamu ya sita ya kufanya biashara saa 24 kwa kuhakikisha uwepo wa watoa huduma za Majisafi na Usafi wa Mazingira.
Pia, amesema kutakuwepo vifaa vya kisasa vya uzibuaji na usafishaji wa mifereji ya majitaka utakaosaidia kuweka eneo la Kariakoo safi muda wote.
“Tumejipanga kuhudumia wafanyabiashara na wageni wanaokuja kupata huduma katika eneo hili la Kariakoo kwa kuhakikisha uwepo wa vifaa vya kisasa vya kuweza kuzibua na kusafisha line kubwa za Majitaka zinazoanzia inch 6 hadi 24.
Pamoja na kufungua Mabwawa ya Majitaka Vingunguti na Kurasini kuanza kufanya kazi saa 24 kwa ajili ya kupokea magari yaajitaka,” ameaema Mhandisi Ndibalema.