Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
BILIONI 52 ZAIMARISHA MIFUMO YA MAJITAKA KINONDONI
19 Jun, 2025
BILIONI 52 ZAIMARISHA MIFUMO YA MAJITAKA KINONDONI

Kaya zaidi ya 11,000 katika kata za Kawe, Kunduchi, Mbezi juu na Wazo katika Wilaya ya Kinondoni wameanza kuunganishiwa huduma ya Majitaka katika makazi yao ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa  Majitaka uliosimamiwa na kutekelezwa  na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) kwa gharama ya Shilingi Bilioni 52

Akizungumzia zoezi hilo ndugu, Hemed Ally mkazi wa Mtaa wa Kilongawima amesema zoezi la maunganisho ya huduma ya majitaka linaloendelea kwasasa linawapa matumaini ya kuboresha afya za wakazi na kupunguza changamoto za kutokea kwa magonjwa ya mlipuko.

"Tumeona kazi kubwa inayoendelea kwasasa, tulisubiri hatua hii ianze mapema Ili mradi utakapoanza kufanya kazi utunufaishe kwa wakati, Wananchi tumeupokea mradi huu kwani utaenda kutupa uhakika wa afya bora na kuepusha utiririshaji wa Majitaka ovyo mtaani." ameeleza ndugu, Hemed.

Msimamizi wa mradi huo kwa upande wa DAWASA, Mhandisi Mabula Jeremiah ameeleza kuwa mwitikio wa Wananchi kujiunga na huduma ni kubwa tangu zoezi lianze.

"Baada ya kukamilisha mradi  tumekamilisha maunganisho katika mifumo ya majitaka kwa zaidi ya Kaya 2,100 na kazi inaendelea katika maeneo ya Mbezi beach A, Kata ya Kawe, Kilongawima Kata ya Kunduchi na Kata ya Mbezi juu 
Kwa kasi hii tunategemea maunganisho yote 11,400 ambao ni wanufaika wa mradi huu watafikiwa" ameeleza Mhandisi Mabula.

Utekelezaji wa Mradi wa Usafi wa Mazingira Mbezi beach umehsisha uchimbaji na ulazaji wa bomba kwa umbali wa Kilomita 101, ujenzi wa vituo viwili vya kusukuma majitaka, ujenzi wa chemba 2383 pamoja na Mtambo wa kisasa wa kuchakata majitaka utakaojengwa eneo la Kilongawima.