CHALINZE YAKABIDHI VIFAA KWA WATEJA WAPYA
23 Oct, 2024

Zoezi la ugawaji wa vifaa vya maunganisho mapya kwa wateja 200 linaendelea katika ofisi za Mkoa wa kihuduma DAWASA Chalinze.
Wananchi walioomba huduma ya maji kutoka katika Kata ya Bwilingu,Msata, Mdaula, Mkange, Lugoba, Miono, Fukayosi na Mbwewe wamepokea vifaa hivyo na zoezi la kuunganishia wateja hao linaendelea.
Mamlaka inaendelea na zoezi la ugawaji wa vifaa vya maunganisho mapya kwa wateja wote walioleta maombi ya kupatiwa huduma ya majisafi katika maeneo yote yanayohudumiwa na DAWASA Dar es Salaam na Pwani.
Kwa msaada na taarifa zaidi wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja namba 0800110064 (Bure) au 0752 801178 (DAWASA Chalinze)