DAWASA, BUNGE ZAUNGANISHA NGUVU KUIMARISHA HUDUMA ZA MAJI DAR ES SALAAM

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (DAWASA) imeshiriki kikao maalum cha Bunge la Sauti ya Raia ambalo limewakutanisha wawakikilishi wa wananchi kutoka Mitaa na Kata mbalimbali za Mkoa wa Dar es Salaam ili kuwasilisha na kusikiliza changamoto za huduma na kupata elimu sahihi ya huduma za DAWASA.
Taasisi hii ya binafsi ya Bunge la Sauti ya Raia imefanyika kwa lengo kuu la kuwakutanisha Wananchi na Wawakilishi kutoka sehemu mbalimbali kama fursa ya kutoa, kupokea maoni na kupata majibu ya changamoto za kihuduma kutoka DAWASA.
Wananchi wawakilishi kutoka katika maeneo yafuatayo walishiriki; Tabata Kinyerezi, Segerea, Gerezani, Kariakoo, Ilala, Buguruni, Pugu, Mbezi, Kibamba, Ubungo, Magomeni, Kinondoni, Tegeta, Mbweni, Temeke, Tuangoma, Mbagala, Kijichi, Kipunguni, Zingiziwa, Msongola na Chanika.
Bunge la Sauti ya Raia ni Taasisi binafsi iliyobuniwa na kuanzishwa mkoani Tanga kwa lengo la kuunganisha wananchi na taasisi za serikali katika kuibua na kutatua kero na changamoto katika jamii kwa kutumia kauli mbiu ya Tanzania Bila ya Mabango ya Kero Inawezekana ambapo huwasilishwa kwa kutumia njia za redio, televisheni na mitandao ya kijamii.