Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
DAWASA FIKISHENI HUDUMA YA MAJI MAENEO YA PEMBEZONI ZAIDI - MHE MAKALA
15 Jul, 2024
DAWASA FIKISHENI HUDUMA YA MAJI MAENEO YA PEMBEZONI ZAIDI - MHE MAKALA

Katibu wa itikadi, uenezi na mafunzo ya vijana wa Chama cha Mapinduzi Taifa, Comrade Mhe. Amos Gabriel Makalla ameitaka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kufikisha huduma ya majisafi kwa wakazi wa maeneo ya pembezoni mwa jiji la Dar es Salaam ikiwemo eneo la Msumi wilayani Ubungo.

Aneyasema hayo wakati wa ziara yake katika Mkoa wa Dar es salaam alipotembelea miradi ya Majisafi baada ya kutembelea tenki la maji  Mshikamoni ambapo ameeleza kuwa wananchi wa maeneo ya pembezoni wana haki sawa na wale wanaoishi katikati ya jiji ya kupata huduma ya majisafi na salama.

"Hii sio mara yangu ya kwanza kutembelea tenki hili nimewahii kuja nikiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam lakini naona sasa kuna mabadiliko haswa baada ya ziara ya Waziri wa Maji, Wananchi wameanza kuona mabadiliko ya upatikanaji wa huduma ya maji mpaka wananchi wanauliza kimetokea nini, tusisubiri viongozi waje kututatulia changamoto ambazo ziko ndani ya uwezo wetu” alisema Mhe. Makalla

"Nimeambiwa kuna mpango wa muda mfupi na muda mrefu ili kusaidia upatikanaji wa huduma ya maji ambapo awali ni kuchimba visima vitatu na baadae kujenga tenki litakalo pata maji kutoka Ruvu moja kwa moja, hivyo niwatake mkamilishe kwa wakati bila kusukumwa" alisema Mhe. Makalla

Hata hivyo ameipongeza Mamlaka kwa kugawa vifaa na kuanza kuunganishia huduma ya maji kwa wananchi waliokwisha lipia katika maeneo ya Wazo na Kibamba.

Naye Mbunge wa jimbo la Kibamba Mhe. Issa Mtemvu ameipongeza DAWASA kwa kuendelea kuboresha huduma na kusisitiza kuboresha zaidi upatikanaji wa huduma ya majisafi katika maeneo ya pembezoni ikiwemo maeneo ya Makabe, Msumi, Msakuzi na Mpiji Magoe.

Kwa upande wa Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA  Mhandisi Mkama Bwire amemshukuru Comrade Makalla kwa kutembelea mradi wa Maji Mshikamano na kuahidi kuwa magizo yaliyotolewa ili kuboresha huduma ya majisafi katika jiji la Dar es Salaam na Pwani yatatekelezeka kwa wakati.