Wizara ya Maji

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)

TIRA Logo
DAWASA INAVYOWAFIKIA WATEJA NA MAJI KIGANJANI
09 Sep, 2025
DAWASA INAVYOWAFIKIA WATEJA NA MAJI KIGANJANI

Wananchi mbalimbali katika maneno ya Kibamba na Mivumoni wamepongeza utaratibu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), kuwarahisishia huduma kwa kuwapelekea vifaa vya maunganisho mapya majumbani na kuwaungia huduma kwa wepesi.

Zaidi ya kaya 80 kutoka mitaa ya Mpiji Magohe, Mloganzila, Kiluvya Madukani, Makurunge, Nyakasangwe, Tegeta A na Madale wamefikiwa na kupatiwa vifaa hivyo.

Ndugu Abiud Shayo, mkazi wa Kata ya Kiluvya amesema utaratibu huu unapunguza umbali wa wateja kufata vifaa wenyewe katika ofisini za DAWASA lakini unaharakisha zoezi la kuunganishwa na huduma ya maji kwa kutumia muda mfupi.

"Tunapunguza gharama nyingi kufatilia vifaa wenyewe katika ofisi za DAWASA na kupunguza umbali, muda mwingi sasa tutaendelea na shughuli zetu za kawaida huku tukiwa na uhakika wa kupatiwa vifaa na kuunganishwa na huduma ya maji, kwa hili niwapongeze DAWASA," amesema Ndugu Shayo.

Mhandisi Mkashida Kavishe, Meneja wa Mkoa wa Kihuduma DAWASA Kibamba amesena lengo kubwa la kupeleka vifaa kwa wananchi ni pamoja na kusogeza huduma zaidi na kuharakisha zoezi la maunganisho ya majisafi kwa wateja ambao wameshakamilisha taratibu zote za kupatiwa huduma.

"Utaratibu huu utarahisisha uunganishaji wa huduma ya maji kwa wananchi, watumishi wetu wapo mtaani kuhakikisha kila aliefikia vigezo vya kupata huduma anapatiwa vifaa vyake na Kuunganishiwa huduma kwa haraka, hii itatusaidia kuongeza idadi ya wananchi tunaowahudumia," amesema Mhandisi Kavishe.