Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
DAWASA KAWE MTAANI MAADHIMISHO WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA
07 Oct, 2024
DAWASA KAWE MTAANI MAADHIMISHO WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) katika kuadhimisha Wiki kimataifa ya Huduma kwa Wateja yenye kauli mbiu “Ni zaidi ya Matarajio”, Mkoa wa Kihuduma Kawe umefanya zoezi la kutembelea wateja nyumba hadi nyumba, kwa lengo la kusikiliza kero zao na kutoa suluhisho kwa haraka. 

Lengo kuu ni kuwahudumia wateja kwa viwango vya juu zaidi ya matarajio yao, kwa kuhakikisha huduma zinapatikana kwa urahisi na kwa ufanisi. Zoezi hili limeimarisha mahusiano kati ya DAWASA na wateja wake, huku likitoa elimu kwa wananchi kuhusu huduma zinazopatikana na jinsi ya kuzifikia kwa urahisi. 

Hii ni sehemu ya juhudi za DAWASA kuhakikisha utoaji wa huduma bora kwa wateja wake.