DAWASA KUIMARISHA HUDUMA YA MAJI MTONI

Mafundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) wakiendelea na kazi ya matengenezo katika bomba kubwa la usambazaji maji la inchi 16 eneo la Mtoni kwa lengo la kuimarisha upatikanaji wa huduma ya maji kwa wakazi wanaohudimiwa na bomba hilo.
Matengenezo hayo yanayotarajiwa kukamilika Jumamosi, Mei 17 2025 yataimarisha upatikanaji wa huduma ya maji wa maeneo ya Mtoni Mtongani, Mtoni Aziz Ally, Mtoni Kichangani, Tandika, Azimio, Kijichi, Mbagala Sabasaba, Mbagala Makuka, Mbagala Bughudadi, Mbagala Mwisho, Zakiem, Mbagala Kibonde Maji, na Mbagala rangi tatu,Kizuiani,Kipati,Mwanamtoti, Mianzini
DAWASA inaendelea kutoa rai kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa za upotevu wa maji katika maeneo yao kupitia kituo cha huduma kwa wateja namba 0800110064 ambayo ni bure au kupitia mitandao ya kijamii ya Mamlaka.