DAWASA MAPINGA YAONGEZA WIGO WA UTOAJI HUDUMA KWA WATEJA

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)imeendelea na zoezi la kuongeza wigo wa upatikanaji wa huduma ya majisafi kwa wananchi ili kuhakikisha lengo la Serikali la kufikisha huduma ya majisafi kwa wananchi wote linafikiwa kikamilifu.
Mojawapo ya jitihada ambazo Mamlaka imefanya ni pamoja na kuendelea na zoezi la ugawaji wa vifaa vya maunganisho mapya kwa wateja takribani 93 wa maeneo Mapinga, Kerege, Kitonga, Vikawe, Kiharaka na Kerege Amani.
Ugawaji wa vifaa vya maunganisho mapya ya maji uliendana sambamba na utoaji wa elimu ya utunzaji bora wa miundombinu ya maji pamoja na kuwashirikisha kwenye mikakati wa kuzuia upotevu wa maji.
Wateja walikumbushwa juu ya umuhimu wa kuwa na mawasiliano ya karibu na Mamlaka kwa lengo la kupata taarifa na ufafanuzi wa mambo mbalimbali yahusuyo huduma. Kwa mawasiliano ya DAWASA Mapinga wateja wameaswa kutumia namba 0734359622 au 181 Bure