DAWASA MIONGONI MWA WASHIRIKI KONGAMANO LA WANAWAKE WAHANDISI NCHINI
21 Aug, 2024

Sehemu ya watumishi wahandisi Wanawake wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) katika kongamano la 9 la wahandisi Wanawake lililoandaliwa na Taasisi ya wahandisi Tanzania linalofanyika kuanzia tarehe 21 - 22 Agosti, 2024 - jijini Dar es Salaam.
Kongamano hilo limefunguliwa na Waziri wa Ujenzi, Mhe. Innocent Bashungwa limebeba kaulimbiu ya "Nguvu ya Wahandisi Wanawake katika kuendeleza maendeleo kuelekea ulimwengu endelevu."