DAWASA NYUMBA KWA NYUMBA KWA WADAIWA HUDUMA ZA MAJI MIKOCHENI

Watumishi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) wameingia mtaani kuendesha zoezi la ufuatiliaji wa malipo ya huduma za maji kwa wateja wenye madeni ya bili za maji ya muda mrefu maeneo ya Kawe katika Wilaya ya Kinondoni.
Zoezi limeenda sambamba na kusikiliza na kutatua changamoto za kihuduma, pamoja na ufuatiliaji wa hali ya huduma za maji katika maeneo mbalimbali.
Zoezi limetekelwzwa katika mitaa ya Mikocheni B, Barabara ya Bima, Mtaa wa Wastaafu, Mtaa wa Msikitini, Mtaa wa Mazingira, Mtaa wa Shule, Mtaa wa Hashimu Rungwe pamoja na Viwandani.
Mamlaka inaendelea kuwafikia wananchi na wateja kupitia kampeni ya DAWASA mtaa kwa Mtaa ikiwa na lengo la kuboresha mahusiano na jamii ikiwa ni msingi wa upatikanaji wa huduma bora.