DAWASA YATOA SOMO UMUHIMU WA ULIPAJI BILI KWA WAKATI
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)Mkoa wa Kihuduma Ilala umeendelea na zoezi la kupita nyumba kwa nyumba na kuwahimiza wateja kuhusu ulipaji wa ankara za maji kwa wakati ili kuiwezesha Mamlaka kuendelea kutoa huduma bora na endelevu kwa wananchi.
Zoezi hili linalotekelezwa kila mwezi, linalenga kuiwezesha Mamlaka kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kupitia makusanyo ikiwemo upanuzi wa huduma, maboresho ya miundombinu kupunguza upotevu wa maji na kuongeza uhakika wa upatikanaji wa majisafi kwa wateja wote.
Sambamba na zoezi hilo, wateja wamehimizwa kuhusu njia sahihi za uhifadhi na udhibiti wa upotevu wa maji, njia za ulipaji wa ankara za maji kupitia(Benki, mitandao ya simu na App) pamoja na utoaji wa taarifa kupitia namba ya Huduma kwa Wateja 181 (bure).
