Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
DAWASA, OFISI YA MKUU WA MKOA DAR ES SALAAM WAFANYA USAFI
13 Jan, 2025
DAWASA, OFISI YA MKUU WA MKOA DAR ES SALAAM WAFANYA USAFI

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imeshiriki katika zoezi la kufanya usafi wa Mazingira lililofanyika katika Wilaya ya Ilala ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Mkoa wa Dar es Salaam kuhamasisha wanananchi kufanya usafi na kutunza mazingira katika maeneo yao.

Watumishi mbalimbali wa DAWASA walishiriki kufanya usafi katika mitaa mbalimbali wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert John Chalamila ambaye aliambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama, Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo, Mkurugenzi wa Jiji pamoja na watumishi wa Mkoa na Jiji la Dar es Salaam.

Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam amesisitiza uboreshaji wa miundombinu ya utunzaji na ukusanyaji wa taka katika maeneo maalum ili kutengeneza mbolea na nishati jambo litakaloongeza fursa za ajira pamoja na usafi wa mazingira ili Jiji la Dar es Salaam liendelee kuwa safi na kivutio cha uwekezaji na utalii.

Washiriki wengine wa zoezi hilo ni pamoja na TANESCO, NEMC na Wafanyabiashara wa maeneo ya wilaya ya Ilala.