Wizara ya Maji

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)

TIRA Logo
DAWASA UKONGA YAIMARISHA USHIRIKIANO USOMAJI MITA SHIRIKISHI
16 Feb, 2026
DAWASA UKONGA YAIMARISHA USHIRIKIANO USOMAJI MITA SHIRIKISHI

Watumishi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) wa Mkoa wa Kihuduma Ukonga wameendelea na zoezi la usomaji mita shirikishi katika maeneo mbalimbali ya Kihuduma. 

Zoezi hilo linaendelea kutekelezwa na DAWASA kwa kuwafikia wateja na kushirikiana katika usomaji wa mita za maji kwa lengo la kuimarisha ushirikiano na kuboresha huduma. 

Usomaji mita shirikishi unahusisha uhakiki katika usomaji mita ili wateja kujiridhisha na kuhakikisha wanalipia kiwango halisi walichotumia sambamba na kuongeza uwazi na uaminifu kati yao na Mamlaka.

Aidha, zoezi hili linasaidia kudhibiti upotevu wa maji, kuhamasisha matumizi bora ya maji na kupunguza malalamiko ya wateja yanayohusu bili.

Zoezi la usomaji mita shirikishi linakwenda sambamba na utoaji wa elimu mbalimbali juu ya huduma zinatolewa na DAWASA, njia za malipo, udhibiti wa upotevu wa maji na mawasiliano rasmi ya Mamlaka katika uboreshaji wa huduma za maji kwa wananchi wa Dar es Salaam na Pwani.