Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
DAWASA UKONGA YAINGIA MTAANI WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA
08 Oct, 2024
DAWASA UKONGA YAINGIA MTAANI WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA

Watumishi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (DAWASA) Mkoa wa Kihuduma wa Ukonga wanaendelea kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja kwa zoezi la kuwatembelea na kuwafikia wateja wake mtaa kwa mtaa kwa lengo la kusikiliza, kupokea na kutatua changamoto za kihuduma walizonazo katika maeneo yao.

Zoezi hilo linaendelea kufanyika katika maeneo yote ya kihuduma ya Kata za Pugu, Majohe, Gongolamboto, Pugu Stesheni na Chanika.

Maadhisho ya wiki ya huduma kwa wateja hufanyika kila mwaka kuanzia tarehe 7 hadi 11 Oktoba ambapo mwaka huu kauli mbiu inasema "Ni Zaidi ya Matarajio".