Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
DAWASA, WATENDAJI SEKTA YA MAJI WASHIRIKI UWASILISHAJI BAJETI YA MAJI
09 May, 2025
DAWASA, WATENDAJI SEKTA YA MAJI WASHIRIKI UWASILISHAJI BAJETI YA MAJI

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Mkama Bwire, ameungana na Viongozi na Watendaji wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maji katika kikao cha Bunge cha kujadili wasilisho la makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Maji kwa Mwaka wa fedha 2025/2026, lililowasilishwa na Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb).

Kupitia hotuba hiyo, Waziri aliainisha mafanikio makubwa yaliyopatikana katika Sekta ya maji katika kipindi cha Miaka minne chini ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita, pamoja na vipaumbele na mpango wa utekelezaji kwa mwaka ujao wa fedha ikiwemo utekelezaji wa miradi 1,539 ya Majisafi Nchini kote.

DAWASA itaendelea kuhakikisha upatikanaji wa huduma endelevu ya Majisafi na Usafi wa Mazingira ndani ya eneo lake la kihuduma.