Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
DAWASA YAENDELEA KUBORESHA USAFI WA MAZINGIRA SINZA, MWENGE HADI MIKOCHENI
28 Aug, 2025
DAWASA YAENDELEA KUBORESHA USAFI WA MAZINGIRA SINZA, MWENGE HADI MIKOCHENI

Mafundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), wakiendelea na uboreshaji wa mazingira katika maeneo mbalimbali ya Jiji yenye mtandao wa majitaka ikiwemo, Kariakoo, Mikocheni, Sinza na Mwenge ili kuboresha ufanisi wake.

Lengo la maboresho haya ya mara kwa mara ni kumaliza changamoto ya uzibaji inayosababishwa na shughuli za kibinadamu ikiwemo utupaji wa taka ngumu kama vile chupa za plastiki, nguo chakavu, mawe na matairi, hali inayopelekea uchafuzi wa mazingira kwa kutiririsha majitaka mitaani.

Mamlaka inasisitiza wananchi kutoa taarifa mapema pindi wanapoona uchafuzi wa mazingira ili changamoto iweze kutatuliwa, pamoja na kuboresha ulinzi wa miundombinu ya majitaka.