DAWASA YAFIKA MAJUMBANI KUTATUA CHANGAMOTO YA HUDUMA YA MAJI

Katika kuhakikisha huduma ya majisafi inaendelea kuwa imara kwa wateja kwa muda wote, Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mkoa wa Kihuduma Mapinga umetembelea na kukagua hali ya upatikanaji wa huduma ya maji kwa wateja wanaohudumiwa katika eneo hilo.
Zoezi hilo ambalo limeongozwa na Meneja wa Mkoa wa Kihuduma DAWASA Mapinga Mhandisi Redempta Bigirwa, lililenga kubaini changamoto zilizopo zinazokwamisha baadhi ya wananchi wa maeneo ya Mapinga kukosa maji au kupata huduma kwa msukumo mdogo.
Katika zoezi hilo, timu ya wataalamu kutoka DAWASA Mapinga walikagua hali ya upatikanaji wa huduma kwa wateja wa maeneo ya Kiharaka, Kiembeni, Kerege na Nyakahamba na kuwaeleza wateja wa maeneo hayo mikakati iliyopo ya kuboresha huduma ya maji kwa wateja wote.
Mamlaka inaendelea na jitihada za kuhakikisha upatikanaji wa maji unakuwa imara kwa wateja wote wanaohudumiwa kwa lengo la kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita ya kumtua ndoo Mama kichwani.