Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
DAWASA YAHITIMISHA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA, 761 WAUNGANISHIWA HUDUMA
15 Oct, 2024
DAWASA YAHITIMISHA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA, 761 WAUNGANISHIWA HUDUMA

Katika kuhitimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja Watumishi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) wameendelea na zoezi la kutoa huduma bora na kwa ufanisi kwa wateja kwa kuwasogezea huduma kwenye makazi sambamba na kauli mbiu ya mwaka huu isemayo 
Ni zaidi ya Matarajio 

Hayo yamebainishwa na Meneja wa Usambazaji Maji Mhandisi Damson Mponjoli wakati wa mahojiano maalum na kipindi maalum kilicholenga kuelezea hitimisho la Wiki ya huduma kwa wateja na tathmini ya huduma za Maji Dar na Pwani.

Ameleeza kuwa hali ya huduma ya maji inazidi kuimarika tofauti na hapo awali ambapo changamoto ya maji ilitokana na mifumo ya uzalishaji zilizopata hitilafu na kusababisha kushuka kwa uzalishaji.

"Hali ya huduma ya maji kwa sasa inaendelea kuimarika tulipata changamoto za kipindi kifupi zilizotokana na mifumo ya uzalishaji kupata hitilafu na kupelekea kushuka kwa uzalishaji wa maji ila kwasasa changamoto imetatuliwa," ameeleza Mhandisi Mponjoli.

Kwa upande wake Meneja huduma kwa wateja Doreen Kiwango amesema kuwa baada ya mteja kuzidisha siku 30 bila kulipa huduma lazima apelekewe notisi ya kusitisha huduma kabla kukatiwa maji.

"Kuhusu kumsitishia mteja huduma ni baada ya kuzidisha siku 30 bila kulipa huduma ila kabla hatujakata tunatuma notisi ya kusitisha huduma na anapewa gharama za kurudishiwa huduma. Ila kwa wale waliositishiwa huduma kwa muda mrefu tunaingia nao mkataba wa kurudishiwa huduma na kulipia kwa awamu," amesema Meneja Kiwango.

Wiki ya huduma kwa wateja huadhimishwa Oktoba 7 - 11 Oktoba kila Mwaka na DAWASA imefanikiwa kuwaunganisha wateja huduma ya Majisafi kwa wateja 761 katika maeneo mbalimbali ya Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani na pia kutatua changamoto za wateja papo kwa hapo.