Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
DAWASA YAIMARISHA HUDUMA HUDUMA YA MAJI KIWANGWA
09 Dec, 2024
DAWASA YAIMARISHA HUDUMA HUDUMA YA MAJI KIWANGWA

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mkoa wa kihuduma Chalinze inaboresha huduma ya Maji katika kata ya Kiwangwa, Wilayani Bagamoyo kwa kulaza bomba la inchi 5 kwa umbali wa kilomita 3.

Kukamilika kwa kazi hiyo kutasaidia kuongeza upatikanaji wa huduma ya maji katika vijiji vinne ambavyo ni Misani, Bago, Msinune na Mwetemo.