DAWASA YAIMARISHA MIUNDOMBINU YA MAJI MBEZI KONOIKE
07 May, 2025

Mafundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mkoa wa kihuduma Ubungo wakiendelea na kazi ya matengenezo katika bomba kubwa la usambazaji maji la inchi 10 eneo la Mbezi Konoike.
Akizungumzia utekelazaji wa kazi hiyo Meneja wa DAWASA Mkoa wa kihuduma Ubungo Mhandisi Damson Mponjoli ameeleza kuwa matengenezo hayo yataimarisha na kuongeza kasi ya upatikanaji wa huduma ya maji kwa wakazi wa maeneo ya Mshikamano kwa Beda, Mshikamano miti miwili, Mshikamano 101, Konoike pamoja na Serikali ya Mtaa Mshikamano.
DAWASA inaendelea kutoa rai kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa za upotevu wa maji katika maeneo yao kupitia kituo cha huduma kwa wateja namba 0800110064 ambayo ni bure au kupitia mitandao ya kijamii ya Mamlaka.