Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
DAWASA YAPONGEZWA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI
02 Mar, 2025
DAWASA YAPONGEZWA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilala, ndugu Said Sidde amepongeza juhudi za Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)katika utekelezaji wa Ilani ya CCM katika sekta ya Maji akisisitiza kuwa baadhi ya miradi ya maendeleo kupitia DAWASA imeleta mabadiliko makubwa kwa wananchi wa wilaya hiyo.

Akizungumza katika kikao kazi kilichokutanisha wenyeviti wa Serikali za mitaa kutoka mitaa 159 wa Wilaya ya Ilala kwa lengo la kuweka mikakati ya kuboresha huduma za Maji pamoja na kuboresha uhusiano.

Ndugu Sidde amesema kuwa utekelezaji wa ilani ya serikali umejidhihirisha kwa vitendo haswa katika kuboresha huduma za Maji kwa wananchi wa Ilala ambao kwa muda mrefu walikumbwa na changamoto kubwa ya upatikanaji wa majisafi na salama.

"Tunaona juhudi za serikali katika kuhakikisha kuwa wananchi wa Ilala wanapata huduma bora za maji. DAWASA imeendelea kuboresha miundombinu ya usambazaji wa maji, na hili ni moja ya mafanikio makubwa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM," amesema ndugu Sidde.

Ndugu Sidde pia ameitaka DAWASA kuendelea kushirikiana na wenyeviti ambao wako kwa niaba ya wananchi ili kutatua changamoto zilizobaki, ikiwemo upanuzi wa mitandao ya maji na uimarishaji wa huduma katika maeneo ya pembezoni. 

Kwa kumalizia, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala amesema kuwa miradi ya Maji inatekeleza ahadi za Serikali za kuhakikisha kuwa kila mwananchi anapata huduma bora za kijamii.