DAWASA YASHIRIKI MKUTANO MKUU WA MAKATIBU MAHSUSI 2024
25 May, 2024

Makatibu Mahsusi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) wamekuwa miongoni mwa washiriki wa Mkutano mkuu wa Mwaka wa Makatibu Mahsusi wa Taasisi za Serikali na binafsi uliofanyika Mkoani Mwanza hivi karibuni.
Mkutano ulikuwa na kauli mbiu ''Mafanikio huanza na uamuzi bora wa utendaji , tutumie muda vizuri kwa kufanyakazi na kuleta tija''.