DAWASA YAWAFIKIA BUZA - KEREZANGE
31 Jul, 2024

Zoezi la kugawa vifaa vya maunganisho mapya kwa wakazi wa maeneo ya Buza,Kurasini,Mashine ya maji,Kerezange,Temeke,Kiwalani,Mzambarauni,Azimio kusini ambao wamekamilisha taratibu za upatikanaji wa huduma ya majisafi, limetekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA).
Zoezi la kugawa vifaa hivyo limefanyika katika ofisi za DAWASA TEMEKE ambapo wateja 54 wamepatiwa vifaa hivyo tayari kwa ajili ya kuunganishwa na huduma ya Majisafi.
Sambamba na Zoezi hilo, DAWASA imetoa elimu ya utunzaji miundombinu ya maji, njia rasmi za kuwasiliana na Mamlaka na malipo ya ankara na huduma nyingine zitolewazo na DAWASA.