Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
DAWASA YAWAKUMBUKA WATOTO WAISHIO MAZINGIRA MAGUMU GOBA
17 May, 2024
DAWASA YAWAKUMBUKA WATOTO WAISHIO MAZINGIRA MAGUMU GOBA

Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira Dar es salaam(DAWASA) imekabidhi mahitaji ya kibinadamu katika kituo cha watoto wanaoishi katika mazingira magumu kilichopo mtaa wa Goba, Kata ya Goba wilaya ya Ubungo.

Kituo hicho kina jumla ya watoto 40 kinamilikwa na mtu binafsi na kinapokea watoto kuanzia umri wa 5 hadi 17

Msaada huo uliotolewa ni sehemu ya jitihada za mamlaka katika kutambua na kujaliuwepo na umuhimu wa makundi haya maalum kwenye jamii.

DAWASA inatoa rai kwa wadau mbalimbali kuendelea kuchangia makundi yenye uhitaji katika Jamii.