Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
DAWASA YAWEKA KAMBI KILEMELA - WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA
07 Oct, 2024
DAWASA YAWEKA KAMBI KILEMELA - WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kupitia Mkoa wa kihuduma DAWASA Mapinga imefungua dawati la huduma kwa Wateja katika ofisi ya Kitongoji cha Kilemela - Kata ya Mapinga kwa lengo la kusikiliza changamoto za kihuduma kwa Wananchi wa maeneo hayo. 

Kupitia dawati hilo pia litasaidia kutatua changamoto za huduma ikiwa ni pamoja na kushughulikia changamoto za upatikanaji wa huduma, utoaji wa kumbukumbu namba kwa wateja waliokamilisha taratibu za kihuduma, kupokea taarifa za uvujaji wa maji na taarifa nyingine muhimu za kihuduma.

Mamlaka imejipanga kutembelea na kufanya shughuli mbalimbali katika wiki hii ya huduma kwa wateja 2024 iliyobeba kauli mbiu isemayo "Above and Beyond"