DAWASA YAWEKA KAMBI MWENGE KUSIKILIZA WANANCHI
30 Mar, 2025

Wananchi mbalimbali wameendelea kujitokeza katika Banda la Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) eneo la Stendi Kuu ya Mabasi Mwenge na kwa ajili ya kupata elimu ya huduma za Maji pamoja na kutatuliwa changamoto za kihuduma.
DAWASA imeungana na Taasisi za Umma na binafsi zilizohudhuria tukio maarufu la Mnada wa wafanyabiashara katika Wilaya ya Kinondoni lililoandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni kwa kushirikiana na Kituo cha habari EFM kinachofanyika tarehe 28 hadi 30 Machi, 2025.