Wizara ya Maji

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)

TIRA Logo
DAWASA YAWEKA MKAZO UBORESHAJI MIUNDOMBINU YA MAJI CHALINZE
14 Sep, 2026
DAWASA YAWEKA MKAZO UBORESHAJI MIUNDOMBINU YA MAJI CHALINZE

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imefanya ukarabati wa miundombinu ya usambazaji maji katika eneo la Chalinze kwa kubadilisha kipande cha bomba la zamani lenye ukubwa wa inchi 10 lilokuwa linavuja.

Meneja DAWASA Chalinze, Mhandisi Boniface Philemon, amesema hatua hiyo ni sehemu ya jitihada za Mamlaka katika kuboresha miundombinu ya zamani na kuhakikisha huduma ya maji inapatikana kwa uhakika.

 ''Kipande hicho cha bomba kilikuwa kimeanza kuvuja kutokana na miundombinu kuwa ya muda mrefu, hivyo wataalamu wetu wa DAWASA wamechukua hatua ya kukiondoa na kuweka kipande kipya ili kudhibiti upotevu wa maji na kurejesha ufanisi wa mfumo wa usambazaji" amesema Mhandisi Boniface.

Amesema ukarabati wa miundombinu ya zamani unaendelea katika maeneo mbalimbali yanayohudumiwa na DAWASA Mkoa wa Kihuduma Chalinze, ikiwa ni mkakati wa kupunguza changamoto za upotevu wa maji na kuimarisha utoaji wa huduma kwa wananchi.

 Aidha Mamlaka imeendelea kutoa wito kwa wananchi kutoa taarifa kupitia kituo cha huduma kwa wateja namba 181 bure kuhusu miundombinu iliyoharibika ili hatua za ukarabati zimefanyike kwa wakati bila kuathiri upatikanaji wa huduma ya maji kwa wananchi.