Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
GAUWASA WAJA DAWASA "KUCHOTA MADINI" HUDUMA KWA WATEJA
28 Sep, 2024
GAUWASA WAJA DAWASA "KUCHOTA MADINI" HUDUMA KWA WATEJA

Watumishi kutoka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Gairo (GAUWASA) wamefanya ziara ya mafunzo Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kwa lengo la kujifunza zaidi na kubadilishana uzoefu wa uendeshaji na usimamizi bora wa huduma za Majisafi na Usafi wa mazingira. 

Katika ziara hiyo wametembelea Mtambo wa uzalishaji maji Ruvu Juu pamoja na mitambo ya kisasa ya kuchakata takatope kujionea na kujifunza jinsi DAWASA inavyotekeleza shughuli za uzalishaji na usambaji  Majisafi pamoja na huduma za usafi wa mazingira.