HUDUMA YA MAJI YABORESHWA MTAA WA MAFIA - ILALA
14 Mar, 2025

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mkoa wa Kihuduma Ilala wanatekeleza mradi wa kuongeza upatikanaji wa majisafi katika mtaa wa Kongo na Mafia, Ilala.
Zoezi hilo limehusisha uchimbaji na uvushaji wa bomba la maji la inchi 3 kutoka kwenye bomba la inchi 6 lililopo mtaa wa Kongo kwa umbali wa mita 80, ili kuboresha upatikanaji wa huduma ya majisafi.
Kukamilika kwa mradi huu kutawezesha wananchi wa maeneo ya Mafia, Jangwani na Likoma kuwa na uhakika wa kupata huduma ya majisafi kulinganisha na awali ambapo hawakuwa na uhakika wa kupata maji.
Utekelezaji wa mradi huu umefikia asilimia 90 na unatarajia kunufaisha wananchi zaidi ya 100 wa mitaa tajwa.