Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
HUDUMA YA MAJI YAENDELEA KUIMARIKA DAR NA PWANI
16 Dec, 2024
HUDUMA YA MAJI YAENDELEA KUIMARIKA DAR NA PWANI

Ni baada ya kukamilika matengenezo Ruvu Juu

Wananchi  wa maeneo ya Mlandizi,Kibaha, Kibamba, Ubungo na Kinyerezi wameanza kupata huduma ya majisafi kufuatia kukamilika kwa matengenezo  katika mtambo wa uzalishaji maji Ruvu Juu yaliyofanyika na kukamilika mapema wiki hii.

DAWASA imeshuhudia uimarikaji huo wakati wa zoezi la kukagua huduma katika baadhi ya Kata na mitaa mbalimbali ndani ya maeneo hayo.

Rahel Cristian, mkazi wa mtaa wa Burula Kimara ameishukuru DAWASA kwa kuhakikisha huduma ya maji imerejea kwani kwa kipindi cha Matengenezo iliwalazimu kununua maji kutoka 
maeneo ya mbali na wengine kutumia maji visima vya watu binafsi ambayo hawakuwa na uhakika wa  ubora wake. 

Baada ya matengenezo kukamilika, huduma inaendelea kuimarika katika maeneo mengine yanayohudumiwa na mtambo wa Ruvu juu.

Zoezi la ufuatiliaji upatikanaji huduma ya maji inaendelea na Watumishi wa DAWASA katika maeneo mbalimbali ili kuhakikisha huduma inamfikia kila Mwananchi.