Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
HUDUMA YA MAJI YAREJEA BOKO NHC
06 Jun, 2024
HUDUMA YA MAJI YAREJEA BOKO NHC

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) kwa kushirikiana na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini *(TARURA) imekamilisha marekebisho ya miundombinu ya mabomba iliyoathiriwa na mvua iliyosababisha kukatika kwa barabara eneo la mto Nyakasangwe na kusababisha ukosefu wa maji kwa wakazi wa Boko NHC na Boko Magereza.

Hali ya huduma imeimarika na wateja wa maeneo ya Boko NHC hadi Boko Magereza wanapata huduma ya maji. 

Endelea kuwasiliana nasi kupitia namba ya huduma kwa wateja 0800110064 (bure) au 
0738 096084 (DAWASA Tegeta).

Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano