HUDUMA YA MAJISAFI YAIMARIKA KIMARA

● Ni baada ya matengenezo ya Mfumo wa umeme kukamilika
Wananchi mbalimbali wa mitaa ya Hawaii, Baruti na Pentagon kata ya Kimara Wilaya ya Ubungo wameanza kupata huduma ya Majisafi kuimarisha kufuatia kukamilika kwa matengenezo ya mfumo wa umeme katika mtambo wa uzalishaji maji Ruvu Juu yaliyokamilika hivi karibuni.
DAWASA imeshuhudia uimarikaji huo wa huduma wakati wa zoeI maalum la kupita katika mitaa mbalimbali ya kihuduma ili kubaini changamoto za Wakazi na kuzitatua.
Ndugu Sauda Abdallah, mkazi wa mtaa wa Hawaii amesema kwa kipindi cha Matengenezo iliwalazimu Wakazi kununua maji kutoka
maeneo ya mbali na wenginekutumia maji ya visima vya watu binafsi.
DAWASA inaendelea kufuatilia hali ya huduma ya maji katika maeneo mbalimbali yanayohudumiwa na mtambo wa Ruvu Juu ili kuondoa changamoto za kihuduma.