KARIAKOO, ILALA NA BUGURUNI WAKUMBUSHWA ULIPAJI WA ANKARA ZA MAJI KWA WAKATI
07 May, 2024

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam na (DAWASA) imetembelea na kuhamasisha ulipaji wa ankara za maji kwa kupita nyumba kwa nyumba wateja waliopo Wilaya Ilala na kutoa elimu ya umuhimu wa wateja kulipa bili zao kwa wakati.
Zoezi hili linalenga kuwakumbusha wateja wajibu wa kulipa ankara kwa wakati na kuwaelekeza njia rahisi za malipo kupitia mitandao ya simu na Benki washirika.
Wateja waliotembelewa ni Wakazi wa maeneo ya Kariakoo, Ilala, Buguruni na katikati ya Jiji.