Wizara ya Maji

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)

TIRA Logo
KATIBU MKUU WIZARA YA MAJI ATUNUKIWA TUZO KUTOKA CHUO CHA TAIFA CHA ULINZI
26 Oct, 2026
KATIBU MKUU WIZARA YA MAJI ATUNUKIWA TUZO KUTOKA  CHUO CHA TAIFA CHA ULINZI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi  Mwajuma  Waziri, ametunukiwa tuzo ya heshima na Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania (NDC, kwa kutambua mchango wake wa kitaaluma na kushiriki  kutoa mhadhara kuhusu nafasi ya sekta ya maji katika maendeleo ya taifa kwa washiriki wa Kozi Na. 15 ya mwaka wa masomo 2026/2027.

Tuzo hiyo inaakisi umuhimu wa kubadilishana maarifa na kuimarisha ushirikiano kati ya Wizara ya Maji na taasisi za kitaaluma katika kujenga uelewa wa pamoja kuhusu mchango wa sekta ya maji katika maendeleo na usalama wa taifa