Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
KAYA 3000 KUIMARISHIWA HUDUMA SALASALA
04 Sep, 2024
KAYA 3000 KUIMARISHIWA HUDUMA SALASALA

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imetekeleza kazi ya kudhibiti upotevu wa maji katika mabomba makuu ikiwemo bomba la inchi 12”   katika eneo la Salasala iliyohusisha udhibiti wa bomba chakavu za muda mrefu.

Kukamilika kwa kazi hii kutasaidia kurejesha na kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji kwa wakazi zaidi ya 3000 wa maeneo ya Kinzudi, Usukumani, Tatedo, Magorofani, Mwakalapa, Ofisi ya Kata ya Goba na Kurungu.