KIBAHA KUONGEZA WIGO WA UTOAJI HUDUMA YA MAJI KWA WANANCHI
14 Jan, 2026
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)Mkoa wa Kihuduma Kibaha imetekeleza zoezi la ugawaji wa vifaa vya maunganisho ya majisafi kwa wananchi wapatao 105 wa maeneo ya Maili moja, Picha ya Ndege, Kwa Mathias, Msangani, Galagaza, Simbani, Mfipa, Miembesaba na Mwendapole.
Zoezi hilo limetekelezwa na Mamlaka kwa lengo la kuboresha upatikanaji wa huduma ya maji kwa wananchi zaidi ya 550 ndani ya mwezi Januari.
Utoaji wa vifaa vya maunganisho umeambatana na elimu ya matumizi sahihi ya maji pamoja na kulinda miundombinu inayosambaza huduma katika maeneo yao.
Wananchi wameshauriwa kuendelea kutumia njia sahihi za kupata huduma za Mamlaka ikiwemo Mawasiliano ya Kituo cha Huduma kwa Wateja kwa namba 181 Bure.
