KIBONDEMAJI WABORESHEWA HUDUMA
24 Feb, 2025

Mafundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) DAWASA Mbagala wakiendelea na kazi ya uboreshaji huduma ya maji kwa wakazi takribani 1,200 wa eneo la Kibondemaji, Wilaya ya Temeke ambao umehusisha ulazaji wa bomba za inchi 3 kwa umbali wa mita 300 sambamba na uwekaji wa toleo la inchi 6.
Kukamilika kwa maboresho haya utakaonufaisha wakazi wa mitaa ya Majimatitu C, Kibondemaji A na Kimbangulile ambayo wanapata huduma ya majisafi kupitia visima vya Nzasa I na Nzasa II.