Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
KING'ONG'O JESHINI WAIMARISHIWA HUDUMA
12 Feb, 2025
KING'ONG'O JESHINI WAIMARISHIWA HUDUMA

Mafundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mkoa wa kihuduma Ubungo wakiendelea na kazi ya uboreshaji wa miundombinu ya maji eneo la King'ong'o Jeshini kwa lengo la kuongeza msukumo wa maji.

Kazi hiyo imehusisha ubadilishwaji wa bomba za inchi mbili (2) hadi mbili na nusu (2½) utakowezesha kuongeza msukumo wa maji kwa wakazi takribani 1,300 wa maeneo ya Jeshini, Mbuyuni, Boom Bekhar, Kwa BC na King'ong'o.