KIPAWA HADI TAZARA WABORESHEWA MIUNDOMBINU YA MAJITAKA.
31 May, 2025

Kazi ya uboreshaji miundombinu ya mfumo wa majitaka ikiendelea eneo la Bakhresa hadi Tazara Nyerere road chini ya usimamizi wa mafundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA).
Uboreshaji wa miundombinu hii unahusha usafishaji wa chemba za kukusanya majitaka pamoja na ujenzi wa mifuniko ya chemba hizo ili kuzuia taka ngumu kuingia na kuongeza ufanisi.
Mamlaka inasisitiza matumizi sahihi ya miundombinu ya Majitaka kwa kuepuka utupaji wa taka ngumu katika mifumo hiyo itakayosababisha kuziba na kupelekea uchafuzi wa mazingira.