KIPUNGUNI B" WABORESHEWA HUDUMA YA MAJI

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imekamilisha kazi ya maboresho ya miundombinu ya huduma ya maji katika eneo la Songas kwa Diwani lililopo Mtaa wa Kipunguni B", Kata ya Kipunguni, Wilaya ya Ilala.
Kazi hiyo iliyotekelezwa na mafundi wa DAWASA Ukonga imehusisha ubadilishaji wa Bomba la inchi 6 kwa lengo la kudhibiti uvujaji wa maji uliosababisha upotevu wa maji hivyo kuathiri msukumo wa upatikanaji wa maji.
Kukamilika kwa kazi hiyo kutaimarisha upatikanaji wa huduma ya maji kwa wakazi takriban 150 wa maeneo ya Kwa Diwani na Bombambili, Kata ya Kipunguni B".
DAWASA inawakumbusha Wananchi kuendelea kutoa taarifa za upotevu wa maji au uharibifu wa miundombinu ya maji kupitia namba za huduma kwa wateja 0800110064 (Bila Malipo) na 0735 20 21 21 (Whatsapp tu).